Friday, January 13, 2012

Hii game ilianza na katiba kumbe wanataka kuturule mpaka 2015 hata sio 2013

"Siasa mbaya maisha mbaya" Nakumbuka baba dan toro akiyasema maneno hayo. Wanasiasa ni wale wale na wanalike kuturule kwa hali na mali. Checki hii game ilianza ma dem days za "tunataka mapinduzi na mareform", ikacome na masaga mob kama saba saba etc then tukajikuta kwa democracia na ma elections ambazo frankly hazijaleta bidii yoyote since wanasiasa waliamua kucheza kadi za ukabila na wanakenya wengi wakajikata sababu ya siasa mbovu {mungu awaweke mahali pema peponi}. Sasa tuko kwa era mpya na after 2002 baba dan toro tukamwambia akalishe, "kenya yetu, Kicc yetu, Kibaki wetu na Nchi yetu" ni maneno niliyosikia wasee wakisherehekea hapo dec 2002. Mwaka wa 2007 ukaja na sote tunajuwa vile kulienda. Coalition ndo hiyo sasa na punde si punde katiba mpya tukapata. Sasa katiba na mwaka wa uchaguzi imekaa ni hesabu ngumu sana maanake inakaa hawa ma grey hair kuna vile walikuwa wamesoma vile hatukuwahi fikiria. 
Koti imeamua election ni march 2012 lakini mimi nakwambia sioni hata election in 2013, actually election ni 20 Aug 2015. Nataka tuichambue katiba pamoja ili tucheki mahali makosa ilifanyika...hakuna mwana siasa atakwambia haya maneno ila mwanakenya mzaledo hapa.
Nataka tuanze na Article 3,9 na 10 ambayo ukitafsiri inaonyesha kuwa uchaguzi in 2012 ni ndoto. Article 10 inasema kuwa bunge inaweza maliza term yake lakini haisemi bunge itakuwa dissolve namna gani maanake section 59 ishaondolewa so prezzo hawezi "vunja" bunge. 
Katiba inasema kuwa Bunge inafaa kuvunjwa baada ya miaka tano kuanzia tarehe waliyo kuwa na kikao cha kwanza. Haya tufanye hesabu sasa, Kikao cha kwanza kilikuwa Januari 16 2008, Ongeza miaka tano hapo na tunapata januari 16 2013. Sasa kwenye hiyo tarehe mpya article 9 na 10 zinasisitiza kuwa uchaguzi lazima ufanyike siku sitini baada ya mbunge kuvunjwa. Tarehe ya uchaguzi sasa inakuwa Marchi 17 2013. Term ya prezzo ina expire miaka tano tangu siku aliyoapishwa usiku, dicemba 29 2007 ongeza miaka tano Unapata Dicember 29 2012. Swali ni, hakutakuwa na prezzo kikatiba kwa miezi tatu?? 
Katiba haikubalishi bunge kuextend term yake mpaka january 15 2013, inasisitiza miaka tano kuanzia 20 aug 2012, hapo vipi??
Inaonekana kuwa hii katiba ililetwa na watu ambao kwa akili zao walikuwa wanapanga njama kuendeleza uongozi mbaya hadi wao wenyewe watakavyotaka kung'atuka uongozini. Tufanye nini sasa??